Mpendwa msomaji:
Je, unaamini kuwa Mwenyezi Mungu ana sifa za ukamilifu?
Kama jibu lako ni ndio… Hapana budi kitabu chake kilichoteremshwa kwa wanadamu nacho kiwe kikamilifu.
Je, unaamini kuwa Manabii na Mitume, amani iwe juu yao, wamelindwa na wapo safi hawafanyi maasi, uzinzi na machafu?
Je, hapo kabla, umeshawahi kufanya mlinganisho baina ya sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Agano la Kale na Quran Tukufu?
Mimi ninakuomba kwa mapenzi yote na moyo safi, tafuta uhakika katika kitabu hiki ambacho huenda kikafungua – Mungu akipenda – nyoyo za wale wenye shauku ya kuokoka na kuongoka.
Samahani ewe mpendwa msomaji, kwa kutaja baadhi ya maandiko ya kimapenzi yenye kutia aibu. Kwani mimi nimenukuu kwa ajili ya kutolea ushahidi tu.