Mitume hawa Ibrahimu, Musa, Isa na Muhammad (Rehema na amani ziwe juu yao) walisali vipi?
Sheikhe Ahmad Deedat, mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu, siku moja, alitembelea Jeddah, Saudi Arabia na kusimulia mojawapo ya jambo lililomtokezea maishani mwake.
Amesem; ilitokea kuwa yeye alikichukua kikundi cha Wakristo na Wayahudi ili watembelee msikiti huko Durban, Afrika Kusini. Walipoingia msikitini, Sheikhe Deedat sio tu alivua viatu vyake, lakini pia alikiomba kile kikundi kifanye kama alivyofanya yeye. Wote wakavua viatu vyao.
Kisha, Deedat akawauliza kama wanajua sababu ya kuvua viatu vyao. Wakajibu, "Hapana." Deedat akawafafanulia: Musa alipokuwa Mlima Sinai, Mungu alimwambia:
"Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu". Kutoka (3:5)
Kile kikundi kilipokuwa kimekaa kwenye benchi na kutazama, Deedat aliwaomba wamruhusu atie udhu. Baada ya kutia udhu, alirudi tena katika kikundi na kufafanua: Udhu huu sio tu una faida kubwa kiafya kama unavyotekelezwa mara tano kwa siku, lakini pia una rejeo la kihistoria. Kisha akanukuu tena:
"Musa na Haruni, na wanawe wakanawa mikono yao na miguu yao ndani yake; hapo walipoingia hema ya kukutania, na hapo walipoikaribia madhabahu, walinawa kama BWANA alivyomwamuru Musa. Kutoka." (40:31-32)
Baada ya Deedat kumaliza sala ya faradhi, alikielekea tena kile kikundi ambacho kwa wakati huo kilikuwa kinawatazama Waislamu wengine wakitekeleza sala zao za suna. Naye akafafanua matendo ya sala, na kutaja kuwa la muhimu zaidi ni kusujudu. Deedat alisema, huku akiziashiria sujudu, namna hii hii ndivyo walivyosali Mitume wote. Akayatia nguvu maelezo yake kwa nukuu:
"Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema," (Mwanzo 17:3)
"Musa na Haruni wakatoka pale walipokuwa mkutano wakaenda hata mlangoni pa hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi; utukufu wa BWANA ukawatokea." (Hesabu 20:6)
"Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la BWANA. Yoshua akapomoka kiusouso hata nchi, naye akasujudu…." (Yoshua 5:14)
Deedat akakiambia kile kikundi: kwa hakika nyinyi mnajua vizuri namna wanavyoabudu Wakristo na Wayahudi na sasa mmeshaona namna wanavyoabudu Waislamu pia.
Dedaat kistaarabu kabisa alikiuliza kile kikundi, namna ya kuabudu ya akina nani inayokaribiana sana na Ukristo? Kile kikundi cha Wakristo na Wayahudi kwa pamoja kilijibu "Bila shaka namna ya kuabudu ya Waislamu ni yenye kuwa karibu zaidi na Ukristo kuliko nyingine."
Leo hii, Wakristo wengi waliosilimu wanashuhudia kuwa kwa sasa wao ni Wakristo bora zaidi kwa kutekeleza jambo hilo. Neno "Mkristo" kwa wepesi kabisa linamaanisha "mfuasi wa Kristo".
Hivyo basi, kwa nini watu hawa ambao kwa sasa wameshaingia Uislamu wanadai kuwa wao ndio wafuasi wa karibu zaidi wa Yesu?
Hebu tufikirie jambo hili kiakili kwa kuyapima yale yanayosemwa na Biblia kuhusiana na Yesu. Kwa mfano, tukisoma Injili tutapata maelezo mengi juu ya Yesu akisali kwa kuweka uso wake ardhini, akiwasalimia wafuasi wake waliomwamini kwa kutumia maelezo ya amani, na kufunga kwa muda mrefu sana.
Kwa hakika wengi wa wale waliokuwa Wakristo hapo zamani wanakiri kuwa, wao walikuwa Waislamu kwa maana zote za neno Uislamu kabla ya kugundua uthibitisho wa imani yao asilia kwa kupitia maandiko ya Quran takatifu iliyofunuliwa kwa mtume wa Mwisho Muhammad (Rehema na amani ziwe juu yake).
"Enyi mlio amini! Rukuuni na msujudu, na muabuduni Mola wenu Mlezi, na tendeni mema, ili mfanikiwe."(QURAN 22:77)
Mnaona wanadamu namna mwitiko wa kibinadamu katika kumpwekesha Mola, Mwitiko ambao hautengani na maumbile ya mwanadamu.
Leo hii, baadhi ya watu wanaodai kuwa wao ni wanafuasi wa njia ya Yesu, Abraham, and Mosa (Rehema na amani ziwe juu yao) wamekengeuka na kuacha hiyo njia. Na kuhusiana na kadhia ya Ukristo, watu wamezua kimakosa njia nyingine kabisa inayomuhusu Nabii Yesu na kwa hiyo wamemfanya Yesu kuwa ni kitu ambacho kamwe hajadai kuwa yeye ni kitu hicho.
Kwa sasa ziulizeni nafsi zenu, kwa uadilifu kabisa, nani hasa anayefuata mfano wa Yesu, leo hii? Kama mnavyojua, Waislamu wanasali kwa kunyenyekea huku mapaji ya nyuso zao yakigusa chini kwa uchache mara tano kwa siku.
Waislamu wanafuata dini ya Yesu; itikadi aliyoisema na kuitekeleza. Vilevile, Waislamu wanamwabudu Mungu yule yule aliyeabudiwa na Yesu; Mungu yule yule wa Ibrahim, Musa na Muhammad (Rehema na amani ziwe juu yao).
Pia, siku zote Waislamu wanasalimiana kwa ibara "Amani iwe juu yenu" vilevile kama alivyofunga Yesu kwa siku 40 huko jangwani Waislamu nao wanafunga mwezi mzima wa Ramadhani.
Mwisho, acha tunyenyekee na kusali kama walivyosali mitume wote hawa.
Tunakualikeni katika mtandao wetu mje mpakue kitabu cha kufundisha sala.